RC CHALAMILA ATAKA MWAROBAINI WA FOLENI DAR UPATIKANE
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amefanya kikao kazi na wadau mbalimbali wa usafirishaji na kuelekeza kuundwa kwa kamati maalumu ya kuratibu kwa haraka namna ya kushughulikia changamoto ya foleni au msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam ambapo kamati hiyo itaratibiwa na katibu Tawala wa Mkoa huo Ndg Abdul Mhinte lengo likiwa ni kupunguza au kumaliza kero hiyo. Akizungumza Jijini Dar es Salaam mara baada ya kikao kazi hicho kilichokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo LATRA, Mamlaka ya bandari, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Viongozi wa madereva malori na daladala pamoja na uwakilishi kutoka Mkoa wa Pwani, hivyo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema ukuaji wa bandari ya Dar es Salaam pamoja na uhitaji wa bandari kavu eneo la jirani na bandari ni miongoni mwa mambo yanayochangia msongamano wa magari katikati ya Jiji hilo, hivyo timu hiyo itashauri namna bora ya kumaliza changamoto hizo RC Chalamila ameongeza kuwa uwepo wa mizani ya kupimia magari kwenye...