Posts

Showing posts from May, 2026

INDICATIVE EXCHANGE RATES TODAY MAY 28th, 2026

Image
 

RC CHALAMILA AKUTANA NA GAVANA WA MKOA WA KHOMAS NAMIBIA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila Mei 26,2026 amekutana na Gavana wa Mkoa wa Khomas Namibia ofisi kwake Ilala boma Jijini Dar es Salaam. Akiupokea ujumbe huo wa Mhe Sam Nujoma Gavana wa Mkoa wa Khomas akiwa ameambatana na Mr Titus Shikongo Balozi wa Namibia Tanzania pamoja na Matheus Olavi msaidizi wa Gavana Mkuu wa Mkoa alipata wasaa wa kufanya mazungumzo wakijadili. Aidha Gavana na wenzake waliweza kutembelea Bandari ya Dar es Salaam, SGR, na Makumbusho ya Taifa ambapo aliweza kujionea shughuli za kiuchumi zinazoendelea na historia ya Afrika hususani harakati za mapambano ya kulikomboa bara la Afrika. Mwisho Gavana huyo bado yuko katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo anatarajia kuendelea kutembelea maeneo mengine ya Mkoa huo.

TARURA YAPATA DOLA MILIONI 65 KUTEKELEZA MIRADI YA DHARURA

Image
Serikali imeiwezesha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupata dola milioni 65 kwa ajili ya utekelezaji wa matengenezo ya miundombinu ya barabara kupitia mfuko wa dharura (CERC). Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo katika mradi wa ujenzi wa daraja lenye urefu wa Mita 22 pamoja na barabara za maingilio zenye urefu wa Mita 290 kwenye barabara ya Ndovelwa yenye urefu wa Km. 20.2 katika Manispaa ya Tabora. Mhandisi Seff amesema fedha hizo ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia uliotolewa kufuatia tathmini ya uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua za El-Nino za mwaka 2024. Amesema tathmini hiyo ilibaini maeneo mengi ya barabara yaliyoharibiwa na hivyo kuhitaji matengenezo ya haraka ili kurejesha mawasiliano na huduma kwa wananchi. “Miradi hii inatekelezwa nchi nzima na kwa wastani utekelezaji wake umefikia asilimia 70. Kazi zote zinatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 2026,” Alis...

TANZANIA KUJIIMARISHA KUWA KITOVU CHA UTAFITI KATIKA KUKABILIANA NA MAJANGA

Image
SERIKALI imesema inaendelea kujipanga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utafiti katika kukabiliana na majanga katika ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika Mashariki, hatua itakayosaidia kuimarisha mifumo ya tahadhari na uokoaji. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi, wakati wa ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga.  Ziara hiyo ya siku tano inayofanyika jijini Maputo nchini Msumbiji kuanzia Mei 25 hadi 29, 2026, inalenga kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu matumizi ya teknolojia za kisasa, tafiti na mifumo ya utoaji wa taarifa za tahadhari mapema ili kupunguza athari za majanga. Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Yonazi alisema Tanzania imeendelea kujenga uwezo wake katika kukabiliana na majanga kupitia uwekezaji katika tafiti na matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo mifumo ya kidijitali na akili bandia (AI), hali ina...

ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI SASA NI DIGRII AU DIPLOMA, TIDO MHANDO AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUREJESHA HADHI YA SEKTA NCHINI

Image
  Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Bw. Tido Mhando, amewataka Waandishi wa Habari nchini kutafakari upya wajibu wao katika kuijenga jamii kupitia maudhui yenye tija, akieleza kuwa ipo haja ya kurejesha hadhi na nguvu ya taaluma hiyo katika kujenga fikra na maendeleo ya taifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bw. Mhando amesema pamoja na JAB kusimamia utoaji wa ithibati kwa kuzingatia vigezo vya elimu na sheria, bado kuna umuhimu wa Waandishi wa Habari kuendelea kujengewa uwezo kupitia mafunzo ya kkitaaluma.  “Tukitazama baadhi ya vyombo vyetu vya habari, iwe ni magazeti, redio au televisheni, mambo ya kufikirisha kwa kiasi kikubwa yamepungua. Waandishi wa Habari wanapaswa kutafakari kama hiyo ndiyo taswira wanayotaka kuiacha katika jamii ya Watanzania,” amesema. Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuunda mtazamo wa jamii, hivyo kuna wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayotolewa yanajenga uelewa, yanakuza maendeleo na yanalinda masl...

TANZANIA, URUSI ZAJADILI MIKATABA YA KUBADILISHANA WAHALIFU NA KUHAMISHA WAFUNGWA

Image
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ndugu Abdulrahaman Mshamu, ameongoza kikao cha kupitia mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirikisho la Urusi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kisheria na mapambano dhidi ya uhalifu wa kimataifa. Mikataba hiyo imejumuisha Mkataba wa Kubadilishana Wahalifu (Extradition Treaty), Mkataba wa Kuhamisha Wafungwa Waliotiwa Hatiani (Transfer of Sentenced Persons) pamoja na Mkataba wa Ushirikiano katika Kulinda Raia dhidi ya Matumizi Mabaya ya Haki ya Kimataifa. Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za Serikali ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Polisi Tanzania pamoja na Jeshi la Magereza Tanzania. Upande wa Shirikisho la Urusi uliwakilishwa na Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Masuala ya Haki ya Urusi, Ndugu Evgeny Bulatov. Akizungumza kat...

MKUTANO WA AfDB 2026 TANZANIA KUGAWANA MKATE WA FEDHA ZA MIRADI YA KIMKAKATI CONGO

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, akizungumza jambo na Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili agenda zinazohusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 61 wa mwaka 2026 wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mwaka wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF),ambapo Mhe. Balozi Omar aliwasilisha taarifa hiyo. Mikutano hiyo itakaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintélé, Congo, Brazzaville. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hamad Omar Bakar (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali ambaye pia katika Muundo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni Gavana Mbadala wa Benki hiyo (Alternate Governor), Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Kaimu Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Kamishna wa Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Viongozi wengine kutoka Ofisi ya Wa...

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3:00 USIKU WA LEO TAREHE 26 MEI 2026

Image
 

MAJAJI 9 WAPYA WA MAHAKAMA YA RUFANI WAAPISHWA LEO NA RAIS SAMIA

Image
  ​DAR ES SALAAM – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 26 Mei, 2026 amewaapisha viongozi wapya tisa wa mhimili wa mahakama walioteuliwa kuhudumu kama Majaji wa Mahakama ya Rufani nchini. ​Hafla hiyo ya kiapo cha uaminifu imefanyika katika Ikulu ya Jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Serikali, mhimili wa Mahakama, pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama. Hatua hii inalenga kuongeza nguvu kazi na kuharakisha kasi ya usikilizaji wa mashauri katika ngazi hiyo ya juu ya maamuzi ya kisheria nchini. ​Majaji walioapishwa rasmi leo mbele ya Mkuu wa Nchi ni pamoja na: ​Mhe. Imani Daud Aboud – Jaji wa Mahakama ya Rufani. ​Mhe. Rabia Hussein Mohamed – Jaji wa Mahakama ya Rufani. ​Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina – Jaji wa Mahakama ya Rufani. ​Mhe. Immaculata Kajetan Banzi – Jaji wa Mahakama ya Rufani. ​Mhe. Cyprian Phocas Mkeha – Jaji wa Mahakama ya Rufani. ​Mhe. Yohane Bokobora Masara – Jaji wa Mahakama ya Rufan...

WAFANYAKAZI TARURA WAHIMIZWA KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA UFANISI LICHA YA MAFANIKIO

Image
‎Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff, amewataka wafanyakazi wa Wakala huo kuendelea kuongeza juhudi, weledi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao licha ya pongezi wanazoendelea kupokea kutoka kwa wananchi kutokana na maboresho ya miundombinu nchini. ‎Mhandisi Seff ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TARURA uliofanyika mkoani Tabora, akisisitiza kuwa mafanikio yaliyopatikana yanapaswa kuwa chachu ya kuongeza bidii zaidi katika kuwahudumia wananchi. ‎"Tunapokea pongezi nyingi kutoka kwa wananchi kutokana na kazi nzuri inayofanywa na TARURA lakini mafanikio hayo yasitufanye turidhike. Tunapaswa kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuongeza juhudi ili kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi", amesema Mhandisi Seff. ‎Ameongeza kuwa anatambua mchango mkubwa wa watumishi wa TARURA nchini kote, akibainisha kuwa jitihada zao zimekuwa na manufaa makubwa tangu kuanzishwa kwa ...

DKT. YONAZI AUPONGEZA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MSUMBIJI KUIMARISHA DIPLOMASIA

Image
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi ameupongeza Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji kwa namna unavyoendelea kutekeleza majukumu yake na kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili. Ametoa pongezi hizo alipotembelea ofisi hizo pamoja na ujumbe alioongozana nao kwa lengo la kushiriki katika ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga unaoendelea kwa siku tano kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mei, 2026 Mjini Maputo Msumbiji. Dkt. Yonazi amezungumza na watumishi wa ubalozi huo na kupokea taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi iliyotolewa na Mwambata fedha Bw. Samson Marwa kwa niaba ya Mhe. CP. Hamad Khamis Hamad, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye alikuwa katika majukumu mengine. Aidha, amewashukuru watumishi wa ubalozi huo kwa namna wanavyoendelea kutekeleza majukumu ya msingi huku wakiiwakilisha nchi na kutekeleza diplomasia ya uchumi kw...

LESENI 108 ZATOLEWA KWA WACHIMBAJI WADOGO, ZINGINE 63 KUFUTWA

Image
Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na ushiriki wa wananchi katika Madini kwa kuendelea kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo nchini, hatua inayolenga kuongeza fursa za ajira, kuinua uchumi wa wananchi na kurasimisha shughuli za uchimbaji mdogo. Katika utekelezaji wa hatua hiyo, Serikali tayari imetenga eneo la Nyakafulu, Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita kwa wachimbaji wadogo na kutoa leseni 108 baada ya kufutwa kwa leseni zilizokuwa haziendelezwi ipasavyo. Hatua hiyo imebainishwa bungeni leo Mei 26, 2026 na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa kwa niaba ya Waziri wa Madini wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu maendeleo ya Sekta ya Madini. Akijibu swali la Mbunge wa Mbogwe, Mhe. Fagason Nkingwa aliuliza kuwa ni lini Serikali itatenga maeneo kwa wachimbaji wadogo na kuwapatia leseni za uchimbaji, Dkt. Kiruswa amesema Serikali tayari imetenga eneo la Nyakafulu kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kutoa jumla ya leseni 108 baada ya kufutwa kwa...

MTWARA YAFUNGUA FURSA MPYA KATIKA SEKTA YA CHUMVI

Image
Serikali Mkoa wa Mtwara umeendelea kujidhihirisha kuwa kitovu muhimu cha uwekezaji katika sekta ya chumvi kutokana na uwepo wa fukwe zinazofaa kwa uzalishaji, maboresho ya mazingira ya biashara na ongezeko la uzalishaji linalofikia takribani tani 90 kwa majaruba manne katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji. Kutokana na hatua hiyo, wachimbaji na wazalishaji wa chumvi wameanza kunufaika na fursa mpya za kiuchumi kupitia kuongezeka kwa uzalishaji, ajira na upanuzi wa maeneo ya uzalishaji. Akizungumza katika mahojiano maalum, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Winnifrida Mrema, amesema sekta ya chumvi mkoani humo inaendelea kukua kwa kasi kutokana na kuimarika kwa shughuli za uzalishaji pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchakataji wa chumvi. Amesema maboresho hayo yanalenga kuongeza ubora wa chumvi kwa matumizi ya majumbani, viwandani na mifugo, huku yakichochea ajira kwa wananchi wa maeneo yanayozunguka mashamba ya chumvi. “Mtwara ina mazingira rafiki kwa uzalishaji wa c...