RC CHALAMILA ATAKA MWAROBAINI WA FOLENI DAR UPATIKANE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amefanya kikao kazi na wadau mbalimbali wa usafirishaji na kuelekeza kuundwa kwa kamati maalumu ya kuratibu kwa haraka namna ya kushughulikia changamoto ya foleni au msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam ambapo kamati hiyo itaratibiwa na katibu Tawala wa Mkoa huo Ndg Abdul Mhinte lengo likiwa ni kupunguza au kumaliza kero hiyo. 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam mara baada ya kikao kazi hicho kilichokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo LATRA, Mamlaka ya bandari, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Viongozi wa madereva malori na daladala pamoja na uwakilishi kutoka Mkoa wa Pwani, hivyo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema ukuaji wa bandari ya Dar es Salaam pamoja na uhitaji wa bandari kavu eneo la jirani na bandari ni miongoni mwa mambo yanayochangia msongamano wa magari katikati ya Jiji hilo, hivyo timu hiyo itashauri namna bora ya kumaliza changamoto hizo

RC Chalamila ameongeza kuwa uwepo wa mizani ya kupimia magari kwenye eneo la kurasini pamoja na ubovu wa baadhi ya miundombinu ya barabara zimekuwa pia zikichangia kusababisha msongamano wa magari ambapo amesema kamati hiyo itashauri namna bora ya kushughulikia changamoto hizo na kuja na mipango ya muda mfupi na muda mrefu.

Miongoni mwa mambo ambayo Mkuu huyo wa Mkoa ameyataja kama muongozo kwenye timu hiyo ya wataalamu ni pamoja na upanuzi wa baadhi ya barabara, uwepo wa baranara ya bypass, malori kuanza kufanyakazi saa tatu usiku hadi saa 11 alfajiri hivyo hivyo ameitaka timu hiyo kujiridhisha kwenye mipango hiyo lakini pia kushauri namna bora ya kushughulikia changamoto hiyo

Aidha kupitia kikao hicho wadau wamezungumzia suala la mabasi ya mikoani na nchi jirani kupaki nje ya kituo cha mabasi cha Magufuli ambapo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema wanatarajia kufanya kikao na wamiliki wa mabasi ili kuhakikisha fedha zilizotumika kwenye uwekezaji wa kituo cha mabasi cha Magufuli uweze kuwa na tija

Katika kikao kazi hicho maalumu kilichohitaji uwepo wa viongozi na wadau kutoka Mkoa wa Pwani ili kuweka nguvu za pamoja, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakar Kunenge amewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.

Comments

Popular posts from this blog

RESIDENTS OF IYAGABUYAGA-BUSEGA URGED TO RESPECT WILDLIFE CONSERVATION LAWS

TANZANIA YAKAMILISHA MFUMO WA KUREJESHA HALI BAADA YA MAAFA

RC CHALAMILA MASHINDANO YA AFCON YATUMIKE KIBIASHARA