RAIS SAMIA AMTEUA UMMY MWALIMU KUWA MSHAURI WAKE MPYA
DAR ES SALAAM – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Mshauri wa Rais kuanzia leo, tarehe 02 Juni, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, aliyeteuliwa ni Bi. Ummy Ally Mwalimu ambaye anakuwa Mshauri wa Rais – Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto. Taarifa hiyo imesainiwa na Shaaban Kissu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Comments
Post a Comment