TANZANIA INAPOTEZA MITI 370,000 KILA MWAKA:NAIBU WAZIRI KWAGILWA NA NMB WAJA NA MKAKATI MPYA WA DIRA 2050
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa amewaomba wadau wa maendeleo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kupanda miti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa Benki ya NMB kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati ya pamoja ya hifadhi ya mazingira endelevu, kikao kimefanyika jijini Dodoma. Mhe. Kwagilwa alisema kuwa katika kufikia lengo la upandaji wa miti takriban bilioni mbili lililowekwa kupitia Dira 2050 zinahitajika nguvu za pamoja kati ya Serikali na wadau na kuendelea kuhamasisha jamii kupanda miti kwenye maeneo yao. Alisema ni lazima kuunganisha nguvu za pamoja kushirikiana ili kuifanya nchi kuwa ya kijani kwani hata katika kaulimbiu iliyotumika kwenye Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu inasema ‘Dira 2050; Tuwajibike kukijanisha Tanzania’ ambayo inasisitiza umuhimu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. “Karibu nusu ya eneo la nchi yet...