MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA ANGALIZO LA UPEPO MKALI UKANDA WA PWANI.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la kuwepo kwa upepo mkali unaotarajiwa kufikia kilomita 40 kwa saa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini mwa Bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 20, 2026, maeneo yatakayokumbwa na hali hiyo ni pamoja na mikoa ya:
- Tanga
- Dar es Salaam
- Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia)
- Visiwa vya Unguja na Pemba
Mamlaka imetoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo yaliyotajwa, hususan watumiaji wa bahari kama vile wavuvi na wasafirishaji, kuwa waangalifu na kuchukua hatua stahiki za usalama ili kujiepusha na madhara yanayoweza kusababishwa na upepo huo mkali.


Comments
Post a Comment